Mlonge au Moringa ni miongoni mwa miti muhimu kuliko yote duniani. Mti huu ukuao haraka hupandwa katika maeneo mengi na hutumika kama chakula cha binadamu, lishe ya mifugo, tiba mbadala nakusafisha maji.
i) Majani ya mti wa Moringa ii) Maua ya mti wa Moringa iii) Mbegu za mti wa Moringa1. Virutubishi
Faida na matumizi ya mti wa Moringa
Karibu kila sehemu ya mti wa Moringa inatumika au inalika kama chakula. Majani ndio sehemu kuu ya mti wa Moringa, unaweza kuyala yakiwa mabichi au yakiwa yamepikwa kama mboga yoyote ya majani, na pia unaweza ukayakausha na kuyahifadhi kama unga-unga kwa miezi mingi huku ukitumia kama kiungo kwenye mboga na mchuzi. Pia majani yanaweza kutumika kama lishe bora ya mifugo.
Utafiti wa kisayansi umeonyesha kuwa majani ya Moringa ni chanzo kikubwa cha virutubishi vingi sana. Virutubishi hivi ni pamoja na;
Karibu kila sehemu ya mti wa Mlonge inatumika au inalika kama chakula. Majani ndio sehemu kuu ya mti wa Mlonge, unaweza kuyala yakiwa mabichi au yakiwa yamepikwa kama mboga yoyote ya majani, na pia unaweza ukayakausha na kuyahifadhi kama unga-unga kwa miezi mingi huku ukitumia kama kiungo kwenye mboga na mchuzi.
Pia majani yanaweza kutumika kama lishe bora ya mifugo.
Utafiti wa kisayansi umeonyesha kuwa majani ya Mlonge ni chanzo kikubwa cha virutubishi vingi sana. Virutubishi hivi ni pamoja na;
Vitamini C – Kirutubishi hiki ni muhimu katika kutengeneza kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali. Kiwango chake katika majani ya Mlonge ni zaidi ya mara saba ya ile inayopatikana kutoka kwenye machungwa.
Calcium (madini chuma) – Kirutubishi hiki ni muhimu katika kuimarisha pamoja na kujenga mifupa na meno mwilini. Kiwango chake katika majani ya Mlonge ni mara nne zaidi ya yale yanayopatikana kutoka kwenye maziwa ya ng’ombe.
Protini – Kirutubishi hiki ni muhimu katika kujenga mwili na kuimarisha ngozi. Kiwango chake katika majani ya Mlonge ni mara mbili zaidi ya ile inayopatikana kutoka kwenye maziwa ya ng’ombe.
Vitamini A – Kirutubishi hiki ni muhimu katika kuimarisha macho na kuongeza uwezo wa kuona. Kiwango chake katika majani ya Mlonge ni mara nne zaidi ya ile inayopatikana kutoka kwenye Karoti.
Potassium – Kirutubishi hiki ni muhimu katika kujenga na kuupatia mwili nguvu. Kiwango chake katika majani ya Mlonge ni mara tatu zaidi ya ile ipatikanayo kutoka kwenye ndizi. Maua ya Mlonge yana kiasi kingi cha madini chuma (calcium) na Potassium kwa wingi na yanaweza kuchemshwa au kupikwa na kuliwa kama mboga.
1. Mboga
Majani ya Mlonge huliwa kama mboga nyingine za majani kwa mfano mchicha. Majani yanaweza kuvunwa wakati wa kiangazi ambapo mboga nyingine hazipatikani. Pia matunda mateke ya Mlonge huweza kutumika kama mboga, hutayariswa kama maharage mabichi (machanga). Matunda yakikomaa hutoa mbegu ambazo zinaweza kutumika kama njegere au kukaangwa kama karanga.

2. Mafuta
Mafuta kutoka kwenye mbegu za mti wa Moringa huweza kutumika katika kupikia na kuwasha katika nyumba. Pia hutumika sana kwenye viwanda katika utengenazaji wa sabuni na bidhaa za urembo. Mafuta hukamuliwa kutoka kwenye mbegu kama ambavyo alizeti hukamuliwa.

3. Lishe ya Mifugo
Majani ya Mlonge huliwa na ng’ombe, mbuzi, kondoo, sungura na kuku. Mbegu huliwa na kuku pamoja na wanyama wengine kwenye jamii ya ndege.
Majani ya Mlonge huliwa na ng’ombe, mbuzi, kondoo, sungura na kuku. Mbegu huliwa na kuku pamoja na wanyama wengine kwenye jamii ya ndege.
4. Pambo la nyumba
Mti wa Mlonge hupandwa kwa wingi kwenye bustani kama ua au mti wa kivuli na hutumika katika upambaji. Pia miti ya mlonge ikipandwa karibu karibu inaweza kutumika kama ukuta/fensi.
Mti wa Mlonge hupandwa kwa wingi kwenye bustani kama ua au mti wa kivuli na hutumika katika upambaji. Pia miti ya mlonge ikipandwa karibu karibu inaweza kutumika kama ukuta/fensi.
5. Chanzo cha kipato
Mti wa Mlonge ukitumiwa vizuri ni chanzo kizuri cha kipato. Mfano ni uuzaji wa miche ya mti wa moringa na utengenezaji wa bidhaa zitokanazo na moringa kama vile mafuta, sabuni na kadharika.
Mti wa Mlonge ukitumiwa vizuri ni chanzo kizuri cha kipato. Mfano ni uuzaji wa miche ya mti wa moringa na utengenezaji wa bidhaa zitokanazo na moringa kama vile mafuta, sabuni na kadharika.
6. Tiba mbadala
Mlonge ni mti muhimu sana katika utabibu kama tiba mbadala, majani, maua, mbegu na mizizi yake hutumika sana katika kutibu magonjwa mbalimbali na maelezo yake ni kama yafuatavyo;
Mlonge ni mti muhimu sana katika utabibu kama tiba mbadala, majani, maua, mbegu na mizizi yake hutumika sana katika kutibu magonjwa mbalimbali na maelezo yake ni kama yafuatavyo;
(a) Majani:
(b) Mbegu:
(c) Unga wa Mlonge:
Tumia kijiko kimoja cha chakula ndani ya uji, au ndani ya juisi ya matunda kikombe kimoja (robo lita) juisi uliyotengeneza mwenyewe, au katika maji ya uvuguvugu kijiko kimoja kikombe kimoja cha maji (robo lita) kutwa mara tatu au unaweza pia kuongeza kijiko kimoja cha unga wa mlonge kwenye mboga ya aina yoyote au katika wali. Tumia kwa mwezi mmoja mpaka mitatu au tumia tu muda wote kama kinga ya mwili wako dhidi ya magonjwa.
(d) Magome:
Matumizi mengineyo
Miti ya Moringa ikipandwa shambani huweza kuwa msaada kwa mimea ipandwayo pamoja nayo kama vile maharage. Pia Moringa ikipandwa bustanini husaidia kupunguza joto la moja kwa moja kufikia mimea kama vile mboga mboga na kupunguza uwezekano wa mboga kusinyaa au kukauka. Mti wa Moringa unaota katika mazingira yote, kwenye ukame na meneo yenye maji. Angalizo huchukuliwa kuhakikisha kuwa maji hayatuami kwenye mti kwasababu maji yakituama kwenye miti ya mlonge huweza kusababisha ugonjwa na kufanya mizizi ioze. Karibu aina zote za udongo zinafaa kwa mti wa Moringa. Mbegu, kipande cha tawi na hata mzizi vinaweza kutumika kuotesha mti wa moringa.

Namna ya kupanda mti wa Moringa
I. Mbegu
Mbegu iliyokomaa ya mti wa Moringa hulowekwa siku moja kabla ya kuoteshwa, kama maji sio tatizo mbegu inaweza kupandwa moja kwa moja kwenye udongo baada ya kuchimba shimo, weka maji na kisha changanya udongo na samadi angalau kilo tano kabla ya kupanda mbegu halafu endelea kumwagilia katika miezi ya mwanzo. Baada ya angalau siku kumi na tano mbegu inatakiwa iwe imeshachipua. Pia unaweza kuotesha mbegu za Moringa katika vifuko kwenye kitalu kisha kuhamishia shambani baada ya kuota.
II. Kipande cha tawi
Vipande vya tawi lililo komaa huweza kutumika katika kupanda mti wa Moringa, hivi hupandwa eidha moja kwa moja shambani au kwenye vifuko katika kitalu. Kama ukipandwa moja kwa moja angalau robo moja ya tawi inatakiwa ipandwe kwenye udongo, usimwagilie maji mengi sana kwani inaweza kusababisha kuoza.

No comments:
Post a Comment